Na wanakuuliza fatwa kuhusiana na wanawake. Sema: Mwenyezi Mungu anawatolea fatwa juu yao, na yale mnayosomewa katika Kitabu hiki kuhusu mayatima wanawake ambao hamuwapi kile walichoandikiwa, na mnapenda kwamba muwaoe, na kuhusu wanyonge katika watoto, na kwamba muwasimamie mayatima kwa uadilifu. Na chochote mnachofanya katika heri, basi hakika Mwenyezi Mungu anaijua vyema.