Kwani huwaoni wale waliokatazwa kunong'onezana, kisha wakayarudia yale yale waliyokatazwa, na wakanong'ona juu ya mambo ya dhambi, na ya uadui, na ya kumuasi Mtume? Na wakikujia, hukuamkua sivyo anavyokuamkua Mwenyezi Mungu. Na husema katika nafsi zao: 'Mbona Mwenyezi Mungu hatuadhibu kwa haya tuyasemayo?' Basi Jahannamu itawatosha; wataingia humo! Na hayo ndiyo marejeo maovu yaliyoje!