Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Al-Kahf 18:32 ۞ واضرب لهم مثلا رجلين جعلنا لاحدهما جنتين من اعناب وحففناهما بنخل وجعلنا بينهما زرعا ٣٢

Ukurasa 297 · Juzuu 15

۞ وَٱضۡرِبۡ
لَهُم
مَّثَلٗا
رَّجُلَيۡنِ
جَعَلۡنَا
لِأَحَدِهِمَا
جَنَّتَيۡنِ
مِنۡ
أَعۡنَٰبٖ
وَحَفَفۡنَٰهُمَا
بِنَخۡلٖ
وَجَعَلۡنَا
بَيۡنَهُمَا
زَرۡعٗا
٣٢
Na wapigie mfano wa wanaume wawili: mmoja wao tulimpa vitalu viwili vya mizabibu, na tukavizungushia mitende, na kati yake tukatia mimea ya nafaka.
reading-goal:continue-reading

Soma q-and-a.tafsir

Ibn Kathir (Abridged)

The Example of the Rich Idolators and the Poor Muslims

After mentioning the idolators who were too arrogant to sit with the poor and weak among Muslims, showing off before them with their wealth and noble lineage, Allah then gives a parable for them of two men, one of whom Allah gave two gardens of g

…

The Example of the Rich Idolators and the Poor Muslims

After mentioning the idolators who were too arrogant to sit with the poor and weak among Muslims

…
Tazama tafsirs

Soma related-content

32. Na wapigie mfano wa wanaume wawili: mmoja wao tulimpa vitalu viwili vya mizabibu, na tukavizungushia mitende, na kati yake tukatia mimea ya nafaka. 33. Na hivyo vitalu viwili vikatoa mazao yake, wala hapana kitu katika hayo kilichotindikia. Na ndani yake tukapasua mito. 34. Naye alikuwa na mazao mengi. Basi akamwambia mwenzake naye akibishana naye: Mimi nimekushinda wewe kwa mali na nguvu za watu! 35. Na akaingia kitaluni kwake, huku anajidhulumu nafsi yake. Akasema: Sidhani kabisa kuwa haya yatawahi kuharibika milele. 36. Wala sidhani kuwa hiyo Saa (ya Kiyama) itatokea. Na ikiwa nitarudishwa kwa Mola wangu Mlezi, bila ya shaka nitapata marejeo bora zaidi kuliko haya. 37. Mwenzake akamwambia kwa kubishana naye: Je, unamkufuru aliyekuumba kutokana na udongo, tena kutokana na tone la manii, kisha akakufanya mwanamume aliye sawasawa? 38. Lakini Yeye Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi. Wala simshirikishi Mola wangu Mlezi na yeyote. 39. Na lau kuwa ulipoingia kitaluni kwako, ungelisema: Mashaallah (alitakalo Mwenyezi Mungu huwa)! Hakuna nguvu yoyote isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Ikiwa unaniona mimi nina mali kidogo zaidi na watoto kuliko wewe. 40. Basi huenda Mola wangu Mlezi akanipa kilicho bora kuliko kitalu chako, na akakitumia balaa kutoka mbinguni kwa hivyo kikageuka kuwa ardhi tupu inayoteleza. 41. Au maji yake yakazama (katika ardhi), basi usiweze kuyatafuta ukayapata. 42. Basi, yakateketezwa matunda yake, akabaki akipinduapindua viganja vyake, kwa vile alivyoyagharamia, huku miti yake imebwagika juu ya chanja zake. Akawa anasema: Laiti nisingelimshirikisha Mola wangu Mlezi na yeyote! 43. Wala hakuwa na kikundi cha kumnusuru badala ya Mwenyezi Mungu, wala mwenyewe hakuweza kujinusuru. 44. Huko ulinzi ni wa Mwenyezi Mungu wa Haki tu. Yeye ndiye mbora zaidi wa malipo, na wa mwisho ulio bora zaidi.

- Swahili Translation - Rowad Translation Center

reading-goal:continue-reading

Maelezo na Tafakari

reflection-not-available

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia