Na walimwekea Mwenyezi Mungu fungu katika mimea na wanyama alioumba, wakasema: 'Hii ni sehemu ya Mwenyezi Mungu - kwa madai yao - na hii ni ya washirikishwa wetu.' Basi vile vilivyokuwa vya washirikishwa wao, havimfikii Mwenyezi Mungu, vile vilivyokuwa vya Mwenyezi Mungu, huwafikia washirikishwa wao. Ni uovu mno hayo wanayoyahukumu.