Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani. Na shikeni Swala, na toeni Zaka, na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwaondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba ya Mtume, na kukusafisheni sawasawa.