Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Yusuf 12:78 قالوا يا ايها العزيز ان له ابا شيخا كبيرا فخذ احدنا مكانه انا نراك من المحسنين ٧٨

Ukurasa 244 · Juzuu 13

قَالُواْ
يَٰٓأَيُّهَا
ٱلۡعَزِيزُ
إِنَّ
لَهُۥٓ
أَبٗا
شَيۡخٗا
كَبِيرٗا
فَخُذۡ
أَحَدَنَا
مَكَانَهُۥٓۖ
إِنَّا
نَرَىٰكَ
مِنَ
ٱلۡمُحۡسِنِينَ
٧٨
Wakasema: Ewe Mheshimiwa! Hakika huyu anaye baba mzee sana. Kwa hivyo mchukue mmoja wetu badala yake. Hakika sisi tunakuona wewe ni katika watu wazuri.
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Ibn Kathir (Abridged)

Yusuf's Brothers offer taking One of Them instead of Binyamin as a Slave, Yusuf rejects the Offer

When it was decided that Benyamin was to be taken and kept with Yusuf according to the law they adhered by, Yusuf's brothers started requesting clemency and raising compassion in his heart for them,

قَال
…

Yusuf's Brothers offer taking One of Them instead of Binyamin as a Slave, Yusuf rejects the Offer

When it was decided that Benyamin was to be taken and

…
Tazama Tafsir

Soma katika Muktadha

69. Na walipoingia alimokuwa Yusuf, alimkumbatia kakaye na akasema: Mimi hakika ndiye yule kaka yako. Basi usihuzunike kwa yale waliyokuwa wakiyafanya. 70. Na alipokwishawatayarishia mahitaji yao, akakitia kikopo cha kunywea maji katika mzigo wa kakaye huyo, kisha mwenye kunadi akanadi: Enyi msafara! Hakika nyinyi ni wezi! 71. Wakasema huku wamegeuka kuwaelekea, “Kwani mmepoteza nini?” 72. Wakasema: Tumepoteza kopo la mfalme. Na atakayenijia nalo, atapewa shehena nzima abebayo ngamia. Nami ni mdhamini juu ya hilo. 73. Wakasema: Tallahi! Hakika mlikwishajua vyema kwamba sisi hatukuja kufanya uharibifu katika nchi hii, wala sisi si wezi. 74. Wakasema: Basi malipo yake ni nini ikiwa nyinyi ni waongo? 75. Wakasema: Malipo yake ni kwamba yule ambaye litapatikana katika shehena lake, basi huyo ndiye malipo yake. Hivyo ndivyo tunavyowalipa madhalimu. 76. Basi akaanza na mizigo yao kabla ya mzigo wa kakaye. Kisha akalitoa katika mzigo wa kakaye. Hivyo ndivyo tulivyompangia njama Yusuf. Hakuwa ni wa kumzuia kakaye kwa sheria ya mfalme huyo isipokuwa Mwenyezi Mungu akitaka. Tunamuinua daraja tumtakaye. Na juu ya kila ajuaye yupo ajuaye zaidi. 77. Wakasema: Akiwa ameiba huyu, basi hakika kakaye vile vile aliiba hapo zamani. Lakini Yusuf akaliweka hilo kisiri katika moyo wake wala hakulionyesha kwao. Akasema: Nyinyi ndio mko katika pahali paovu zaidi, na Mwenyezi Mungu anajua zaidi hayo mnayosingizia. 78. Wakasema: Ewe Mheshimiwa! Hakika huyu anaye baba mzee sana. Kwa hivyo mchukue mmoja wetu badala yake. Hakika sisi tunakuona wewe ni katika watu wazuri. 79. Akasema: Mwenyezi Mungu apishe mbali kumshika yeyote yule isipokuwa yule tuliyemkuta naye kitu chetu. Hakika, hapo tutakuwa ni wenye kudhulumu.

- Swahili Translation - Rowad Translation Center

Endelea Kusoma

Maelezo na Tafakari

Huna maelezo au tafakari yoyote kuhusu aya hii.

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia