Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Luqman 31:7 واذا تتلى عليه اياتنا ولى مستكبرا كان لم يسمعها كان في اذنيه وقرا فبشره بعذاب اليم ٧

Ukurasa 411 · Juzuu 21

وَإِذَا
تُتۡلَىٰ
عَلَيۡهِ
ءَايَٰتُنَا
وَلَّىٰ
مُسۡتَكۡبِرٗا
كَأَن
لَّمۡ
يَسۡمَعۡهَا
كَأَنَّ
فِيٓ
أُذُنَيۡهِ
وَقۡرٗاۖ
فَبَشِّرۡهُ
بِعَذَابٍ
أَلِيمٍ
٧
Na mtu kama huyo anaposomewa Aya zetu, huzipa mgongo kwa kujivuna, kana kwamba hakuzisikia, au masikioni mwake mna uziwi. Basi mbashirie kuwa atapata adhabu chungu.
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Ibn Kathir (Abridged)

Which was revealed in Makkah

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ

In the name of Allah, the Beneficent, the Merciful

The Doomed are preoccupied with Idle Talk and They turn away from the Ayat of Allah

When Allah mentions the blessed -- who are those who are guided by the Book of Allah and benefit

…

Which was revealed in Makkah

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ

In the name of Allah, the Beneficent, the Merciful

The Doomed are preoccupied wit

…
Tazama Tafsir

Soma katika Muktadha

1. Alif Laam Miim. 2. Hizi ni Aya za Kitabu chenye hekima. 3. Kuwa ni uongofu na rehema kwa wafanyao wema. 4. Wale wanaoshika Swala, na wanatoa Zaka, nao wana yakini na Akhera. 5. Hao ndio walio kwenye uongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, na hao ndio waliofaulu. 6. Na miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu mbali na njia ya Mwenyezi Mungu pasipo kujua, na wanaichukulia ni masihara. Hao watapata adhabu ya kuwafedhehesha. 7. Na mtu kama huyo anaposomewa Aya zetu, huzipa mgongo kwa kujivuna, kana kwamba hakuzisikia, au masikioni mwake mna uziwi. Basi mbashirie kuwa atapata adhabu chungu. 8. Hakika walioamini na wakatenda mema watakuwa na Bustani za neema. 9. Watadumu humo, ni ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kweli. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima. 10. Ameziumba mbingu bila ya nguzo mnazoziona, na ameweka katika ardhi milima ili ardhi isiwayumbishe, na ametawanya humo kila namna ya wanyama, na tumeteremsha maji kutoka mbinguni, na tukaotesha katika ardhi mimea mizuri ya kila namna. 11. Huu ni uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Basi nionyesheni wameumba nini hao wasiokuwa Yeye! Lakini madhalimu wamo katika upotovu ulio dhahiri.

- Swahili Translation - Rowad Translation Center

Endelea Kusoma

Maelezo na Tafakari

Huna maelezo au tafakari yoyote kuhusu aya hii.

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia