Soma na usikilize Sura Ibrahim pamoja na tarjuma yake, tafsir, usomaji wa sauti, maana ya neno kwa neno, na unukuzi pia. Tarjuma ya Rowad Translation Center.
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu
Alif Laam Raa.1 Hiki ni Kitabu tulichokuteremshia ili uwatoe watu kwenye giza mbalimbali uwapeleke kwenye mwangaza, kwa idhini ya Mola wao Mlezi, uwafikishe kwenye Njia ya Mwenye nguvu, Msifika.