Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Hud 11:96 ولقد ارسلنا موسى باياتنا وسلطان مبين ٩٦

Ukurasa 232 · Juzuu 12

وَلَقَدۡ
أَرۡسَلۡنَا
مُوسَىٰ
بِـَٔايَٰتِنَا
وَسُلۡطَٰنٖ
مُّبِينٍ
٩٦
Na hakika tulimtuma Musa pamoja na Ishara zetu na uthibitisho ulio wazi.
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Ibn Kathir (Abridged)

The Story of Musa and Fir`awn

In these verses Allah informs of His sending Musa with His signs and clear proofs to Fir'awn, the king of the Coptic people, and his chiefs.

فَاتَّبَعُواْ أَمْرَ فِرْعَوْنَ

(but they followed the command of Fir`awn.) This means that they followed his path, way and methodo

…

The Story of Musa and Fir`awn

In these verses Allah informs of His sending Musa with His signs and clear proofs to Fir'awn, the king of the Coptic peop

…
Tazama Tafsir

Soma katika Muktadha

96. Na hakika tulimtuma Musa pamoja na Ishara zetu na uthibitisho ulio wazi. 97. Kwa Firauni na waheshimiwa wake. Lakini wao wakafuata amri ya Firauni, na amri ya Firauni haikuwa yenye uongofu. 98. Siku ya Kiyama atawatangulia kaumu yake na atawaingiza Motoni. Na muingio mbaya zaidi ulioje huo unaoingiwa! 99. Nao walifuatishwa laana hapa (duniani) na Siku ya Kiyama. Ni kipawa kibaya zaidi kilichoje walichopewa! 100. Hizi ni katika habari za miji, tunakusimulia. Mingine ipo bado na mingine ilifyekwa. 101. Na Sisi hatukuwadhulumu, lakini wao wenyewe walizidhulumu nafsi zao. Na miungu yao waliyokuwa wakiiomba badala ya Mwenyezi Mungu haikuwafaa kitu ilipokuja amri ya Mola wako Mlezi. Na hiyo miungu haikuwazidishia isipokuwa maangamio tu. 102. Na hivyo ndivyo ulivyo mshiko wa Mola wako Mlezi anapoishika miji inapokuwa imedhulumu. Hakika mshiko wake ni mchungu na mkali. 103. Hakika katika hayo ipo ishara kwa yule anayehofu adhabu ya Akhera. Hiyo ndiyo Siku itakayokusanyiwa watu, na hiyo ndiyo Siku itakayoshuhudiwa. 104. Na wala hatuiahirishi isipokuwa kwa muda unaohisabiwa. 105. Siku hiyo itakapokuja, nafsi yoyote haitazungumza isipokuwa kwa idhini yake. Basi miongoni mwao kutakuwa na walio mashakani na wenye furaha. 106. Ama wale waliojitia mashakani, hao watakuwa Motoni, humo watavuta pumzi na kuitoa kwa ugumu mkubwa. 107. Watadumu humo muda wa kudumu mbingu na ardhi, isipokuwa atakavyo Mola wako Mlezi. Hakika Mola wako Mlezi hutenda atakavyo. 108. Na ama wale waliofurahishwa, wao watakuwa katika Bustani wadumu humo muda wa kudumu mbingu na ardhi, isipokuwa atakavyo Mola wako Mlezi. Hicho ni kipawa kisicho na kikomo. 109. Basi usiwe katika shaka juu ya yale wanayoyaabudu hawa. Hawaabudu isipokuwa kama walivyoabudu baba zao zamani. Na hakika Sisi tutawatimizia fungu lao bila ya kulipunguza.

- Swahili Translation - Rowad Translation Center

Endelea Kusoma

Maelezo na Tafakari

Huna maelezo au tafakari yoyote kuhusu aya hii.

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia