Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Hud 11:32 قالوا يا نوح قد جادلتنا فاكثرت جدالنا فاتنا بما تعدنا ان كنت من الصادقين ٣٢

Ukurasa 225 · Juzuu 12

قَالُواْ
يَٰنُوحُ
قَدۡ
جَٰدَلۡتَنَا
فَأَكۡثَرۡتَ
جِدَٰلَنَا
فَأۡتِنَا
بِمَا
تَعِدُنَآ
إِن
كُنتَ
مِنَ
ٱلصَّٰدِقِينَ
٣٢
Wakasema, "Ewe Nuhu! Umejadiliana nasi, na umekithirisha kutujadili. Basi tuletee hayo unayotuahidi, ikiwa wewe ni miongoni mwa wakweli."
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Ibn Kathir (Abridged)

The People's Request of Nuh to bring the Torment and His Response to Them

Allah, the Exalted, informs that the people of Nuh sought to hasten Allah's vengeance, torment, anger and the trial (His punishment). This is based on their saying,

قَالُواْ ينُوحُ قَدْ جَادَلْتَنَا فَأَكْثَرْتَ جِدَالَنَا

(They

…

The People's Request of Nuh to bring the Torment and His Response to Them

Allah, the Exalted, informs that the people of Nuh sought to hasten Allah's v

…
Tazama Tafsir

Soma katika Muktadha

25. Na hakika, tulimtuma Nuhu kwa kaumu yake, akawaambia, "Hakika mimi ni mwonyaji aliye wazi kwenu. 26. Ya kwamba msimuabudu isipokuwa Mwenyezi Mungu tu. Hakika mimi ninawahofia adhabu ya siku chungu." 27. Basi wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake, "Hatukuoni wewe isipokuwa ni mtu tu mfano wetu, wala hatukuoni wamekufuata isipokuwa wale wetu walio duni, watu wasiokuwa na maoni. Wala hatuwaoni nyinyi kuwa mna ubora wowote kutushinda sisi. Bali tunawadhania nyinyi kuwa ni waongo." 28. Akasema, "Enyi kaumu yangu! Hebu fikirini! Ikiwa mimi ninayo hoja wazi iliyotoka kwa Mola wangu Mlezi, na amenipa rehema kutoka kwake, nayo ikafichwa kwenu. Je, tuwalazimishe kuikubali ilhali nyinyi mnaichukia? 29. Na enyi kaumu yangu! Mimi siwaombi mali kwa ajili ya haya. Mimi sina ujira isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu; na mimi sitawafukuza walioamini. Hakika wao watakutana na Mola wao Mlezi, lakini mimi nawaona mnafanya ujinga. 30. Na enyi kaumu yangu! Ni nani atakayeninusuru kwa Mwenyezi Mungu nikiwafukuza hawa? Basi je, hamkumbuki? 31. Wala siwaambii kuwa nina hazina za Mwenyezi Mungu, wala kuwa mimi ninajua mambo ya ghaibu, wala sisemi: Mimi ni Malaika. Wala sisemi kuhusu wale ambao yanawadharau macho yenu kuwa Mwenyezi Mungu hatawapa heri. Mwenyezi Mungu ndiye anayajua zaidi yaliyo katika nafsi zao. Hapo bila ya shaka nitakuwa miongoni mwa madhalimu." 32. Wakasema, "Ewe Nuhu! Umejadiliana nasi, na umekithirisha kutujadili. Basi tuletee hayo unayotuahidi, ikiwa wewe ni miongoni mwa wakweli." 33. Akasema, "Hakika Mwenyezi Mungu tu ndiye atakayewaletea akitaka. Wala nyinyi si wenye kumshinda. 34. Wala nasaha yangu haitawafaa kitu nikitaka kuwanasihi, ikiwa Mwenyezi Mungu anataka kuwapoteza. Yeye ndiye Mola wenu Mlezi, na kwake mtarejeshwa." 35. Au ndio wanasema, "Ameizua?" Sema, "Ikiwa nimeizua, basi kosa hilo ni juu yangu, na mimi niko mbali sana na makosa myatendayo."

- Swahili Translation - Rowad Translation Center

Endelea Kusoma

Maelezo na Tafakari

Huna maelezo au tafakari yoyote kuhusu aya hii.

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia