Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

At-Tawba 9:95 سيحلفون بالله لكم اذا انقلبتم اليهم لتعرضوا عنهم فاعرضوا عنهم انهم رجس وماواهم جهنم جزاء بما كانوا يكسبون ٩٥

Ukurasa 202 · Juzuu 11

سَيَحۡلِفُونَ
بِٱللَّهِ
لَكُمۡ
إِذَا
ٱنقَلَبۡتُمۡ
إِلَيۡهِمۡ
لِتُعۡرِضُواْ
عَنۡهُمۡۖ
فَأَعۡرِضُواْ
عَنۡهُمۡۖ
إِنَّهُمۡ
رِجۡسٞۖ
وَمَأۡوَىٰهُمۡ
جَهَنَّمُ
جَزَآءَۢ
بِمَا
كَانُواْ
يَكۡسِبُونَ
٩٥
Watawaapia kwa Mwenyezi Mungu mtakaporudi kwao ili muwaachilie mbali. Basi waachilieni mbali. Hakika hao ni najisi, na makazi yao ni Jahannam, kuwa ni malipo kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Ibn Kathir (Abridged)

Exposing the Deceitful Ways of Hypocrites

Allah said that when the believers go back to Al-Madinah, the hypocrites will begin apologizing to them.

قُل لاَّ تَعْتَذِرُواْ لَن نُّؤْمِنَ لَكُمْ

(Say "Present no excuses, we shall not believe you."), we shall not believe what you say,

قَدْ نَبَّأَنَا اللَّ
…

Exposing the Deceitful Ways of Hypocrites

Allah said that when the believers go back to Al-Madinah, the hypocrites will begin apologizing to them.

قُل
…
Tazama Tafsir

Soma katika Muktadha

94. Watawatolea udhuru mtakapowarudia. Sema: Msitoe udhuru; hatutawaamini. Mwenyezi Mungu amekwishatujulisha habari zenu. Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wataviona vitendo vyenu. Kisha mtarudishwa kwa Mjuzi wa ya siri na ya dhahiri; naye atawaambia mliyokuwa mkiyatenda. 95. Watawaapia kwa Mwenyezi Mungu mtakaporudi kwao ili muwaachilie mbali. Basi waachilieni mbali. Hakika hao ni najisi, na makazi yao ni Jahannam, kuwa ni malipo kwa yale waliyokuwa wakiyachuma. 96. Wanawaapia ili muwe radhi nao. Lakini hata mkiwa radhi nao nyiye, basi hakika Mwenyezi Mungu hawi radhi na kaumu wavukao mipaka. 97. Mabedui ndio wenye ukafiri mkubwa zaidi na unafiki, na wameelekea zaidi kutojua mipaka ya yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu juu ya Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kujua zaidi, Mwenye hekima. 98. Na katika Mabedui hao kuna yule anayefikiri kuwa kile anachotoa ni gharama ya bure, na anakutazamieni mambo yawageukie. Mageuko maovu yatakuwa juu yao! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote. 99. Na katika Mabedui kuna yule anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na anakichukulia kile anachotoa kuwa ni cha kumsongeza karibu na Mwenyezi Mungu na cha kupata kwacho dua za Mtume. Ndiyo! Hayo hakika ni mambo ya kuwasongeza karibu. Mwenyezi Mungu atawaingiza katika rehema yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

- Swahili Translation - Rowad Translation Center

Endelea Kusoma

Maelezo na Tafakari

Huna maelezo au tafakari yoyote kuhusu aya hii.

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia