Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

At-Tawba 9:104 الم يعلموا ان الله هو يقبل التوبة عن عباده وياخذ الصدقات وان الله هو التواب الرحيم ١٠٤

Ukurasa 203 · Juzuu 11

أَلَمۡ
يَعۡلَمُوٓاْ
أَنَّ
ٱللَّهَ
هُوَ
يَقۡبَلُ
ٱلتَّوۡبَةَ
عَنۡ
عِبَادِهِۦ
وَيَأۡخُذُ
ٱلصَّدَقَٰتِ
وَأَنَّ
ٱللَّهَ
هُوَ
ٱلتَّوَّابُ
ٱلرَّحِيمُ
١٠٤
Je, hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anakubali toba ya waja wake, na anazichukua sadaka, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kukubali toba, Mwenye kurehemu sana?
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Ibn Kathir (Abridged)

The Command to collect the Zakah and Its Benefits

Allah commanded His Messenger to take Sadaqah from the Muslims' money to purify and sanctify them with it. This Ayah is general, even though some said that it refers specifically to those who mixed good and evil deeds, who admitted to their errors. So

…

The Command to collect the Zakah and Its Benefits

Allah commanded His Messenger to take Sadaqah from the Muslims' money to purify and sanctify them wit

…
Tazama Tafsir

Soma katika Muktadha

100. Na wale waliotangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na wale waliowafuata kwa uzuri, Mwenyezi Mungu aliwaridhia, na wao walimridhia, na amewaandalia Bustani zipitazo mito chini yake, watadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa. 101. Na katika mabedui walio jirani zenu kuna wanafiki; na katika wakazi wa Madina pia wapo wale waliobobea katika unafiki. Wewe huwajui. Sisi tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili, kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa. 102. Na wengine walikiri dhambi zao, walichanganya matendo mema na mengine mabaya. Huenda Mwenyezi Mungu akakubali toba zao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. 103. Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwayo, na waombee dua. Hakika kuomba dua kwako ni utulivu kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote 104. Je, hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anakubali toba ya waja wake, na anazichukua sadaka, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kukubali toba, Mwenye kurehemu sana? 105. Na sema: Tendeni matendo. Na Mwenyezi Mungu atayaona matendo yenu, na Mtume wake, na Waumini. Na mtarudishwa kwa Mwenye kujua siri na dhahiri; basi naye atawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda. 106. Na wapo wengine wanaongojea amri ya Mwenyezi Mungu. Ima atawaadhibu au atawakubalia toba. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua zaidi, Mwenye hekima. 107. Na wapo waliojenga msikiti kwa ajili ya madhara, na ukafiri, na kuwafarikisha Waumini, na pa kuvizia kwa ajili ya wale waliompiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake hapo kabla. Na bila ya shaka wataapa kwamba: 'Hatukukusudia isipokuwa uzuri tu.' Na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa wao hakika ni waongo. 108. Usisimame ndani yake kabisa. Msikiti uliojengwa juu ya msingi wa ucha Mungu tangu siku ya mwanzo unastahiki zaidi wewe usimame ndani yake. Humo wamo wanaume wanaopenda kujitakasa. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wanaojitakasa. 109. Je, mwenye kuweka msingi wa mjengo wake juu ya uchaji utokao kwa Mwenyezi Mungu na radhi zake ni bora zaidi au mwenye kuweka msingi wa mjengo wake juu ya ukingo wa shimo unaoporomoka? Kwa hivyo ukaporomoka naye ndani ya Moto wa Jahannamu? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu madhalimu. 110. Na mjengo wao huo walioujenga hautaacha kuwa shaka katika nyoyo zao mpaka nyoyo zao hizo zikatike vipande vipande. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.

- Swahili Translation - Rowad Translation Center

Endelea Kusoma

Maelezo na Tafakari

Huna maelezo au tafakari yoyote kuhusu aya hii.

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia