Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

As-Sajdah 32:11 ۞ قل يتوفاكم ملك الموت الذي وكل بكم ثم الى ربكم ترجعون ١١

Ukurasa 415 · Juzuu 21

۞ قُلۡ
يَتَوَفَّىٰكُم
مَّلَكُ
ٱلۡمَوۡتِ
ٱلَّذِي
وُكِّلَ
بِكُمۡ
ثُمَّ
إِلَىٰ
رَبِّكُمۡ
تُرۡجَعُونَ
١١
Sema, "Atakufisheni Malaika wa mauti aliyewakilishwa juu yenu; kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu Mlezi."
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Ibn Kathir (Abridged)

Refutation of Those Who think the Resurrection is unlikely to happen

Allah tells us how the idolators thought it unlikely that the resurrection would ever come to pass, and how they said:

أَءِذَا ضَلَلْنَا فِى الاٌّرْضِ

(When we are lost in the earth,) meaning, `when our bodies have been scattered and

…

Refutation of Those Who think the Resurrection is unlikely to happen

Allah tells us how the idolators thought it unlikely that the resurrection would e

…
Tazama Tafsir

Soma katika Muktadha

1. Alif Laam Miim. 2. Huu ni uteremsho wa Kitabu kisichokuwa na shaka yoyote kinachotoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 3. Au wanasema: Amekizua? Bali hiki ni kweli iliyotoka kwa Mola wako Mlezi ili uwaonye watu wasiofikiwa na mwonyaji kabla yako; huenda wakaongoka. 4. Mwenyezi Mungu ndiye aliyeumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake kwa siku sita, na akainuka akawa juu ya Kiti cha Enzi. Nyinyi hamna mlinzi wala mwombezi isipokuwa Yeye tu. Basi, je, hamkumbuki? 5. Anapitisha mambo yote yaliyo baina ya mbingu na ardhi, kisha yanapanda kwake kwa siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu kwa mnavyohesabu nyinyi. 6. Huyu ndiye Mwenye kuyajua yasiyoonekana na yanayoonekana. Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. 7. Ambaye ametengeneza vizuri umbo la kila kitu na akaanzisha kumuumba mtu kwa udongo. 8. Na kisha akajaalia uzao wake utokane na kizazi cha maji dhaifu yanayodharauliwa. 9. Kisha akamtengeneza sawasawa, na akampulizia katika roho yake, na akawajalieni kusikia na kuona, na nyoyo za kufahamu. Ni uchache mnavyoshukuru. 10. Nao walisema: "Kwani tutakapokwishapotelea chini ya ardhi, ni kweli kwamba tutarudishwa katika umbo jipya?" Bali wao wanakufuru kukutana na Mola wao Mlezi. 11. Sema, "Atakufisheni Malaika wa mauti aliyewakilishwa juu yenu; kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu Mlezi."

- Swahili Translation - Rowad Translation Center

Endelea Kusoma

Maelezo na Tafakari

Huna maelezo au tafakari yoyote kuhusu aya hii.

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia