Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

An-Nur 24:17 يعظكم الله ان تعودوا لمثله ابدا ان كنتم مومنين ١٧

Ukurasa 351 · Juzuu 18

يَعِظُكُمُ
ٱللَّهُ
أَن
تَعُودُواْ
لِمِثۡلِهِۦٓ
أَبَدًا
إِن
كُنتُم
مُّؤۡمِنِينَ
١٧
Mwenyezi Mungu anawaonya msirejee tena kufanya kama haya kabisa, ikiwa nyinyi ni Waumini!
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Ibn Kathir (Abridged)

Further Discipline

This is further discipline, in addition to the command to think well of people, i.e., if something unbefitting is mentioned about good people, then one should think well of them, and not feel towards them anything but good. Then if a person has any unsuitable thoughts about them, i

…

Further Discipline

This is further discipline, in addition to the command to think well of people, i.e., if something unbefitting is mentioned about go

…
Tazama Tafsir

Soma katika Muktadha

11. Hakika wale walioleta uongo ni kundi miongoni mwenu. Msifikiri ni shari kwenu, bali hiyo ni kheri kwenu. Kila mtu katika wao atapata aliyoyachuma katika madhambi. Na yule aliyejitwika sehemu yake kubwa miongoni mwao, atapata adhabu kubwa. 12. Kwa nini mlipoisikia habari hii, wanaume Waumini na wanawake Waumini hawakuwadhania wenzao mema, na kusema: Huu ni uzushi dhahiri? 13. Kwa nini hawakuleta mashahidi wanne? Na ilivyokuwa hawakuleta mashahidi wanne, basi hao mbele ya Mwenyezi Mungu ni waongo. 14. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake katika dunia na Akhera, bila ya shaka ingeliwapata adhabu kubwa kwa sababu ya yale mliyojiingiza. 15. Mlipoyapokea kwa ndimi zenu na mkasema kwa vinywa vyenu msiyoyajua, na mlifikiri ni jambo dogo, kumbe mbele ya Mwenyezi Mungu ni kubwa. 16. Na kwa nini mlipoyasikia msiseme: Haitufalii kuzungumza haya. Subhanak! (Umetakasika!) Huu ni uzushi mkubwa! 17. Mwenyezi Mungu anawaonya msirejee tena kufanya kama haya kabisa, ikiwa nyinyi ni Waumini! 18. Na Mwenyezi Mungu anawabainishia Aya mbalimbali. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi, Mwenye hekima. 19. Kwa hakika wale wanaopenda uenee uchafu kwa walioamini, watapata adhabu chungu katika dunia na Akhera. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui. 20. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake, na kuwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mpole, Mwenye kurehemu.

- Swahili Translation - Rowad Translation Center

Endelea Kusoma

Maelezo na Tafakari

Huna maelezo au tafakari yoyote kuhusu aya hii.

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia