Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Al-Qasas 28:82 واصبح الذين تمنوا مكانه بالامس يقولون ويكان الله يبسط الرزق لمن يشاء من عباده ويقدر لولا ان من الله علينا لخسف بنا ويكانه لا يفلح الكافرون ٨٢

Ukurasa 395 · Juzuu 20

وَأَصۡبَحَ
ٱلَّذِينَ
تَمَنَّوۡاْ
مَكَانَهُۥ
بِٱلۡأَمۡسِ
يَقُولُونَ
وَيۡكَأَنَّ
ٱللَّهَ
يَبۡسُطُ
ٱلرِّزۡقَ
لِمَن
يَشَآءُ
مِنۡ
عِبَادِهِۦ
وَيَقۡدِرُۖ
لَوۡلَآ
أَن
مَّنَّ
ٱللَّهُ
عَلَيۡنَا
لَخَسَفَ
بِنَاۖ
وَيۡكَأَنَّهُۥ
لَا
يُفۡلِحُ
ٱلۡكَٰفِرُونَ
٨٢
Na wale waliotamani kuwa pahala pake jana, wakawa wanasema, "Kumbe Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye katika waja wake, na humkunjia amtakaye. Ingelikuwa Mwenyezi Mungu hakutufanyia hisani, angelitudidimiza. Kumbe makafiri hawafanikiwi!"
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Ibn Kathir (Abridged)

How Qarun and His Dwelling Place were swallowed up by the Earth

After telling us about Qarun's conceit and pride in his adornments, and how he was arrogant towards his people and transgressed against them, Allah then tells us how he and his dwelling place were swallowed up by the earth. This was also

…

How Qarun and His Dwelling Place were swallowed up by the Earth

After telling us about Qarun's conceit and pride in his adornments, and how he was arro

…
Tazama Tafsir

Soma katika Muktadha

76. Hakika Qaruni alikuwa katika watu wa Musa, lakini aliwafanyia dhuluma. Na tulimpa hazina ambazo funguo zake zinawatopeza watu wenye nguvu kuzibeba. Watu wake walipomwambia, "Usijigambe! Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wanaojigamba." 77. Na utafute, kwa aliyokupa Mwenyezi Mungu, makazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la duniani. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyokufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya uharibifu katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wafanyao uharibifu. 78. Akasema, "Kwa hakika nimepewa haya kwa sababu ya elimu niliyo nayo." Je, hakujua kwamba Mwenyezi Mungu alikwisha waangamiza, katika vizazi vya walio kabla yake, watu waliokuwa wenye nguvu zaidi kuliko yeye, na wenye makundi makubwa zaidi kuliko yake. Na wahalifu hawataulizwa habari ya dhambi zao." 79. Basi akawatokea watu wake katika pambo lake. Wakasema wale waliokuwa wanataka maisha ya duniani, "Laiti tungelikuwa tunayo kama aliyopewa Qaruni! Hakika yeye ni mwenye bahati kubwa." 80. Na wakasema wale waliopewa elimu, "Ole wenu! Malipo ya Mwenyezi Mungu ni bora kwa mwenye kuamini na akatenda mema. Wala hawatapewa hayo isipokuwa wenye subira." 81. Basi tukamdidimiza yeye na nyumba yake katika ardhi; wala halikuwepo kundi lolote la kumnusuru kando na Mwenyezi Mungu, wala hakuwa miongoni mwa wanaojinusuru. 82. Na wale waliotamani kuwa pahala pake jana, wakawa wanasema, "Kumbe Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye katika waja wake, na humkunjia amtakaye. Ingelikuwa Mwenyezi Mungu hakutufanyia hisani, angelitudidimiza. Kumbe makafiri hawafanikiwi!"

- Swahili Translation - Rowad Translation Center

Endelea Kusoma

Maelezo na Tafakari

Huna maelezo au tafakari yoyote kuhusu aya hii.

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia