Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Al-Mujadilah 58:11 يا ايها الذين امنوا اذا قيل لكم تفسحوا في المجالس فافسحوا يفسح الله لكم واذا قيل انشزوا فانشزوا يرفع الله الذين امنوا منكم والذين اوتوا العلم درجات والله بما تعملون خبير ١١

Ukurasa 543 · Juzuu 28

يَٰٓأَيُّهَا
ٱلَّذِينَ
ءَامَنُوٓاْ
إِذَا
قِيلَ
لَكُمۡ
تَفَسَّحُواْ
فِي
ٱلۡمَجَٰلِسِ
فَٱفۡسَحُواْ
يَفۡسَحِ
ٱللَّهُ
لَكُمۡۖ
وَإِذَا
قِيلَ
ٱنشُزُواْ
فَٱنشُزُواْ
يَرۡفَعِ
ٱللَّهُ
ٱلَّذِينَ
ءَامَنُواْ
مِنكُمۡ
وَٱلَّذِينَ
أُوتُواْ
ٱلۡعِلۡمَ
دَرَجَٰتٖۚ
وَٱللَّهُ
بِمَا
تَعۡمَلُونَ
خَبِيرٞ
١١
Enyi mlioamini! Mkiambiwa: Fanyeni nafasi katika mabaraza, basi fanyeni nafasi. Na Mwenyezi Mungu atakufanyieni nyinyi nafasi. Na mkiambiwa: "Ondokeni", basi ondokeni. Mwenyezi Mungu atawainua wale walioamini miongoni mwenu, na wale waliopewa elimu daraja za juu. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Ibn Kathir (Abridged)

Manners for Assemblies

Allah teaches His servants good manners and orders them to be kind to each other when they are sitting together,

يأَيُّهَا الَّذِينَ ءَامَنُواْ إِذَا قِيلَ لَكُمْ تَفَسَّحُواْ فِى الْمَجَلِسِ

(O you who believe! When you are told to make room in the assemblies,)

فَافْسَحُواْ يَفْس

…

Manners for Assemblies

Allah teaches His servants good manners and orders them to be kind to each other when they are sitting together,

يأَيُّهَا الَّذِ

…
Tazama Tafsir

Soma katika Muktadha

5. Hakika wanaopinzana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, watadhalilishwa kama walivyodhalilishwa wale waliokuwa kabla yao. Na tulikwishateremsha Ishara zilizo wazi. Na makafiri watapata adhabu ya kufedhehesha. 6. Siku atakapowafufua Mwenyezi Mungu, na awaambie yale waliyoyatenda. Mwenyezi Mungu ameyadhibiti, na wao wameyasahau! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu. 7. Kwani huoni kwamba Mwenyezi Mungu anajua vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi? Hauwi mnong'ono wa watu watatu ila Yeye huwa ni wanne wao, wala wa watano ila Yeye huwa ni wa sita wao. Wala wa wachache kuliko hao, wala walio wengi zaidi, ila Yeye yu pamoja nao popote pale walipo. Kisha Siku ya Kiyama atawaambia waliyoyatenda. Hakika Mwenyezi Mungu anajua zaidi kila kitu. 8. Kwani huwaoni wale waliokatazwa kunong'onezana, kisha wakayarudia yale yale waliyokatazwa, na wakanong'ona juu ya mambo ya dhambi, na ya uadui, na ya kumuasi Mtume? Na wakikujia, hukuamkua sivyo anavyokuamkua Mwenyezi Mungu. Na husema katika nafsi zao: 'Mbona Mwenyezi Mungu hatuadhibu kwa haya tuyasemayo?' Basi Jahannamu itawatosha; wataingia humo! Na hayo ndiyo marejeo maovu yaliyoje! 9. Enyi mlioamini! Mnaponong'ona, msinong'one kwa sababu ya mambo ya madhambi, na uadui, na kumuasi Mtume. Bali nong'onezeni kwa kutenda mema na kuacha maovu. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye kwake mtakusanywa nyote. 10. Kwa hakika minong'ono hiyo inatokana na Shetani ili awahuzunishe wale walioamini, na wala haitawadhuru chochote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na juu ya Mwenyezi Mungu tu ndio wategemee Waumini. 11. Enyi mlioamini! Mkiambiwa: Fanyeni nafasi katika mabaraza, basi fanyeni nafasi. Na Mwenyezi Mungu atakufanyieni nyinyi nafasi. Na mkiambiwa: "Ondokeni", basi ondokeni. Mwenyezi Mungu atawainua wale walioamini miongoni mwenu, na wale waliopewa elimu daraja za juu. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda. 12. Enyi mlioamini! Mnaposema siri na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kusemezana kwenu. Hiyo ni heri kwenu na usafi zaidi. Na ikiwa hamkupata cha kutoa, basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe mno, Mwenye kurehemu zaidi. 13. Mnachelea kutanguliza hiyo sadaka kabla ya kusemezana kwenu kwa siri? Ikiwa hamkufanya hayo, na Mwenyezi Mungu akapokea toba yenu, basi simamisheni Sala, na toeni Zaka, na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.

- Swahili Translation - Rowad Translation Center

Endelea Kusoma

Maelezo na Tafakari

Huna maelezo au tafakari yoyote kuhusu aya hii.

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia