Hakika, wamekufuru wale waliosema: 'Hakika, Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryam!' Na hali Masihi mwenyewe alisema: 'Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Kwani, mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu amemharamishia Bustani ya mbinguni, na pahali pake ni Motoni. Na madhalimu hawatakuwa na wowote wa kuwanusuru.