Enyi mlioamini! Yanapomfikia mauti mmoja wenu na akataka kutoa wasia, basi wawepo mashahidi wawili miongoni mwenu ambao ni waadilifu. Na mnapokuwa katika safari, na msiba wa mauti ukawasibu, basi washuhudie wengineo wawili wasiokuwa katika nyinyi. Mtawazuia wawili hao baada ya Swala na waape kwa Mwenyezi Mungu, mkitilia shaka, wakisema: Hatutopokea thamani yoyote kwa haya hata kwa ajili ya jamaa; na wala hatutaficha ushahidi wa Mwenyezi Mungu; hakika hapo tutakuwa miongoni mwa wenye dhambi.