Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Al-Kahf 18:88 واما من امن وعمل صالحا فله جزاء الحسنى وسنقول له من امرنا يسرا ٨٨

Ukurasa 303 · Juzuu 16

وَأَمَّا
مَنۡ
ءَامَنَ
وَعَمِلَ
صَٰلِحٗا
فَلَهُۥ
جَزَآءً
ٱلۡحُسۡنَىٰۖ
وَسَنَقُولُ
لَهُۥ
مِنۡ
أَمۡرِنَا
يُسۡرٗا
٨٨
Na ama yule mwenye kuamini na akatenda mema, basi huyo ana malipo mazuri, nasi tutamwambia lililo jepesi katika amri yetu.
reading-goal:continue-reading

Soma q-and-a.tafsir

Ibn Kathir (Abridged)

His traveling and reaching the Place where the Sun sets (the West)

فَأَتْبَعَ سَبَباً

(So he followed a way.) Ibn `Abbas said that he followed different routes to achieve what he wanted.

فَأَتْبَعَ سَبَباً

(So he followed a way.) Mujahid said that he followed different routes, east and west. According

…

His traveling and reaching the Place where the Sun sets (the West)

فَأَتْبَعَ سَبَباً

(So he followed a way.) Ibn `Abbas said that he followed differen

…
Tazama tafsirs

Soma related-content

83. Na wanakuuliza kuhusu Dhul-Qarnain. Waambie: nitawasomea baadhi ya hadithi yake. 84. Hakika Sisi tulimuimarisha katika ardhi na tukampa katika njia za kila kitu. 85. Basi akaifuata njia. 86. Mpaka alipofika machweo ya jua, akaliona linatua katika chemichemi yenye matope meusi. Na pale akawakuta kaumu fulani. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnain, ima uwaadhibu au uwafanyie uzuri. 87. Akasema: Ama aliyedhulumu, basi tutamuadhibu kisha atarudishwa kwa Mola wake Mlezi, naye atamuadhibu adhabu mbaya zaidi. 88. Na ama yule mwenye kuamini na akatenda mema, basi huyo ana malipo mazuri, nasi tutamwambia lililo jepesi katika amri yetu. 89. Kisha akaifuata njia. 90. Hata alipofika machomozeo ya jua, akaliona linawachomozea kaumu ambao hatukuwawekea pazia ya kuwakinga kutokana nalo. 91. Vivyo hivyo. Na Sisi tulizijua vilivyo habari zake zote. 92. Kisha akaifuata njia. 93. Hata alipofika katikati ya milima miwili, alikuta nyuma yake kaumu ambao walikaribia kutofahamu neno lolote. 94. Wakasema: Ewe Dhul-Qarnain! Hakika Yaajuju na Maajuju wanafanya uharibifu katika ardhi. Basi je, tukupe ujira ili utie baina yetu na baina yao kizuizi? 95. Akasema: Yale ambayo Mola wangu Mlezi ameniimarisha ndani yake ndiyo bora zaidi. Lakini nisaidieni kwa nguvu. Nitaweka baina yenu na baina yao kizuizi imara. 96. Nileteeni vipande vya chuma. Hata alipoijaza sawasawa nafasi iliyo katikati ya milima miwili hiyo, akasema, "Pulizeni moto" mpaka alipokifanya kuwa moto, akasema, "Nileteeni shaba iliyoyeyuka niimimine juu ya chuma hicho." 97. Basi hawakuweza kukikwea, wala hawakuweza kukitoboa. 98. Akasema, "Hii ni rehema kutoka kwa Mola wangu Mlezi. Na itakapokuja ahadi ya Mola wangu Mlezi, atakivunjavunja. Na ahadi ya Mola wangu Mlezi ni ya kweli." 99. Na tutawaacha baadhi yao siku hiyo wachanganyike wao kwa wao, na litapulizwa baragumu, hapo tutawakusanya wote pamoja. 100. Na siku hiyo tutawadhihirishia wazi Jahannamu makafiri waione. 101. Wale ambao macho yao yalikuwa paziani hawanikumbuki, na wakawa hawawezi kusikia.

- Swahili Translation - Rowad Translation Center

reading-goal:continue-reading

Maelezo na Tafakari

reflection-not-available

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia