Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Al-Jathiyah 45:34 وقيل اليوم ننساكم كما نسيتم لقاء يومكم هاذا وماواكم النار وما لكم من ناصرين ٣٤

Ukurasa 502 · Juzuu 25

وَقِيلَ
ٱلۡيَوۡمَ
نَنسَىٰكُمۡ
كَمَا
نَسِيتُمۡ
لِقَآءَ
يَوۡمِكُمۡ
هَٰذَا
وَمَأۡوَىٰكُمُ
ٱلنَّارُ
وَمَا
لَكُم
مِّن
نَّٰصِرِينَ
٣٤
Na itasemwa: 'Leo tunawasahau kama nyinyi mlivyosahau mkutano wa siku yenu hii; na mahali penu ni Motoni, wala hamna wowote wa kuwanusuru.'
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Ibn Kathir (Abridged)

Allah states to us His judgement in His creation on the Day of Resurrection,

فَأَمَّا الَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ الصَّلِحَتِ

(Then, as for those who believed and did good deeds,) Those whose hearts believed and their limbs performed good deeds, in sincerity to Allah and conforming with Islamic l

…

Allah states to us His judgement in His creation on the Day of Resurrection,

فَأَمَّا الَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ الصَّلِحَتِ

(Then, as for those w

…
Tazama Tafsir

Soma katika Muktadha

27. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Na siku itakaposimama Saa ya Kiyama, siku hiyo wataangamia wenye kushikamana na upotovu. 28. Na utauona kila umma umepiga magoti, na kila umma utaitwa kwenda kusoma kitabu chake: Leo mtalipwa mliyokuwa mkiyatenda. 29. Hiki kitabu chetu kinasema juu yenu kwa haki. Hakika Sisi tulikuwa tukiyaandika mliyokuwa mkiyatenda. 30. Ama walioamini na wakatenda mema, Mola wao Mlezi atawatia katika rehema yake. Huko ndiko kufuzu kuliko wazi. 31. Na ama waliokufuru wataambiwa: 'Kwani hamkuwa mkisomewa Aya zangu nanyi mkapanda kichwa, na mkawa watu wakosefu?' 32. Na ikisemwa: Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli na Saa haina shaka, nyinyi mlikuwa mkisema: Hatuijui hiyo Saa, tunadhania dhana tu, wala hatuna yakini. 33. Basi ubaya wa yale waliyoyatenda utawadhihirikia, na yatawafika yale waliyokuwa wakiyafanyia masihara. 34. Na itasemwa: 'Leo tunawasahau kama nyinyi mlivyosahau mkutano wa siku yenu hii; na mahali penu ni Motoni, wala hamna wowote wa kuwanusuru.' 35. Hayo ni kwa sababu nyinyi mlizifanyia mzaha Aya za Mwenyezi Mungu, na maisha ya dunia yakawadanganya. Basi leo hawatatolewa humo wala hao hawatakubaliwa udhuru wao. 36. Basi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa mbingu na Mola Mlezi wa ardhi, na Mola Mlezi wa walimwengu wote. 37. Na ukubwa ni wake Yeye tu, mbinguni na katika ardhi, naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

- Swahili Translation - Rowad Translation Center

Endelea Kusoma

Maelezo na Tafakari

Huna maelezo au tafakari yoyote kuhusu aya hii.

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia