Hakuna kulazimisha katika Dini. Kwani uongofu umekwishapambanuka kutokana na upotovu. Kwa hivyo, anayemkufuru Taaghuut na akamwamini Mwenyezi Mungu, basi bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisichovunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia mno, Mwenye kujua vyema.1