Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Al-Baqarah 2:199 ثم افيضوا من حيث افاض الناس واستغفروا الله ان الله غفور رحيم ١٩٩

Ukurasa 31 · Juzuu 2

ثُمَّ
أَفِيضُواْ
مِنۡ
حَيۡثُ
أَفَاضَ
ٱلنَّاسُ
وَٱسۡتَغۡفِرُواْ
ٱللَّهَۚ
إِنَّ
ٱللَّهَ
غَفُورٞ
رَّحِيمٞ
١٩٩
Kisha miminikeni kutoka pale wanapomiminika watu, na muombeni Mwenyezi Mungu msamaha. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Ibn Kathir (Abridged)

The Order to stand on `Arafat and to depart from it

This Ayah contains Allah's order to those who stand at `Arafat to also move on to Al-Muzdalifah, so that they remember Allah at Al-Mash`ar Al-Haram. Allah commands the Muslim to stand with the rest of the pilgrims at `Arafat, unlike Quraysh who (bef

…

The Order to stand on `Arafat and to depart from it

This Ayah contains Allah's order to those who stand at `Arafat to also move on to Al-Muzdalifah, so

…
Tazama Tafsir

Soma katika Muktadha

197. Hija ni miezi maalumu. Basi anayehirimia Hija ndani yake (miezi hiyo), basi asijamiiane wala asipindukie mipaka wala asibishane katika Hija. Na chochote mnachokifanya katika heri, Mwenyezi Mungu anaijua. Na chukueni masurufu. Na hakika, masurufu (yaliyo) bora zaidi ni ucha Mungu. Na nicheni Mimi, enyi wenye akili ya hali ya juu! 198. Hakuna ubaya wowote juu yenu kutafuta fadhila kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi mtakapomiminika kutoka 'Arafat, mtajeni Mwenyezi Mungu katika Mash'aril Haram (eneo takatifu). Na mtajeni kama alivyowaongoa, ijapokuwa kabla ya hilo mlikuwa miongoni mwa waliopotea. 199. Kisha miminikeni kutoka pale wanapomiminika watu, na muombeni Mwenyezi Mungu msamaha. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. 200. Na mkishatimiza ibada zenu za Hija, mtajeni Mwenyezi Mungu kama mlivyokuwa mkiwataja baba zenu au utajo mkubwa zaidi. Na katika watu kuna wale wanaosema, “Mola wetu Mlezi, tupe duniani!” Naye katika Akhera hana fungu lolote. 201. Na miongoni mwao kuna wale wanaosema, “Mola wetu Mlezi, tupe duniani mema, na Akhera mema, na utulinde kutokana na adhabu ya Moto!” 202. Hao ndio walio na fungu kwa sababu ya yale waliyoyachuma. Na Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.

- Swahili Translation - Rowad Translation Center

Endelea Kusoma

Maelezo na Tafakari

Huna maelezo au tafakari yoyote kuhusu aya hii.

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia