Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Al-Anfal 8:32 واذ قالوا اللهم ان كان هاذا هو الحق من عندك فامطر علينا حجارة من السماء او ايتنا بعذاب اليم ٣٢

Ukurasa 180 · Juzuu 9

وَإِذۡ
قَالُواْ
ٱللَّهُمَّ
إِن
كَانَ
هَٰذَا
هُوَ
ٱلۡحَقَّ
مِنۡ
عِندِكَ
فَأَمۡطِرۡ
عَلَيۡنَا
حِجَارَةٗ
مِّنَ
ٱلسَّمَآءِ
أَوِ
ٱئۡتِنَا
بِعَذَابٍ
أَلِيمٖ
٣٢
Na waliposema: Ewe Mwenyezi Mungu! Ikiwa haya ndiyo haki kutoka kwako, basi tunyeshee mawe kutoka mbinguni, au tujie na adhabu yoyote iliyo chungu.
reading-goal:continue-reading

Soma q-and-a.tafsir

Ibn Kathir (Abridged)

The Quraysh claimed They can produce Something similar to the Qur'an

Allah describes the disbelief, transgression, rebellion, as well as misguided statements that the pagans of Quraysh used to utter when they heard Allah's Ayat being recited to them,

قَدْ سَمِعْنَا لَوْ نَشَآءُ لَقُلْنَا مِثْلَ هَذَآ

(

…

The Quraysh claimed They can produce Something similar to the Qur'an

Allah describes the disbelief, transgression, rebellion, as well as misguided stat

…
Tazama tafsirs

Soma related-content

29. Enyi mlioamini! Mkimcha Mwenyezi Mungu, atawapa kipambanuo, na atawasitiria mabaya yenu, na awafutie dhambi, na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye fadhila kubwa. 30. Na walipokupangia vitimbi wale waliokufuru ili wakufunge, au wakuue, au wakutoe. Na wakapanga vitimbi vyao, naye Mwenyezi Mungu akapanga vitimbi vyake. Na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa wapangao vitimbi. 31. Na wanaposomewa Aya zetu, wao husema: Hakika tumesikia. Lau tungetaka, tungesema mfano wa haya. Haya si chochote isipokuwa ngano za wa mwanzo. 32. Na waliposema: Ewe Mwenyezi Mungu! Ikiwa haya ndiyo haki kutoka kwako, basi tunyeshee mawe kutoka mbinguni, au tujie na adhabu yoyote iliyo chungu. 33. Na Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaadhibu hali ya kuwa uko miongoni mwao, na Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuwaadhibu hali ya kuwa wanaomba msamaha. 34. Lakini wana nini hata Mwenyezi Mungu asiwaadhibu, na hali ya kuwa wanawazuilia watu Msikiti Mtakatifu, wala wao hawakuwa ndio walinzi wake? Bali walinzi wake si isipokuwa wacha Mungu tu, lakini wengi wao hawajui. 35. Na hakukuwa kuswalia kwao kwenye hiyo Nyumba (Al-Kaaba) isipokuwa ni kupiga miunzi na makofi. Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyokuwa mkikufuru. 36. Hakika wale waliokufuru hutoa mali zao ili waizuilie Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watazitoa, kisha zitakuwa majuto juu yao, kisha watashindwa. Na wale waliokufuru watakusanywa kwenye Jahannam. 37. Ili Mwenyezi Mungu awapambanue waovu kutokana na wazuri, na awaweke waovu juu ya waovu wengine, na awarundike wote pamoja, na awatie katika Jahannam. Hao ndio waliohasirika.

- Swahili Translation - Rowad Translation Center

reading-goal:continue-reading

Maelezo na Tafakari

reflection-not-available

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia