Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Al-An-Am 6:100 وجعلوا لله شركاء الجن وخلقهم وخرقوا له بنين وبنات بغير علم سبحانه وتعالى عما يصفون ١٠٠

Ukurasa 140 · Juzuu 7

وَجَعَلُواْ
لِلَّهِ
شُرَكَآءَ
ٱلۡجِنَّ
وَخَلَقَهُمۡۖ
وَخَرَقُواْ
لَهُۥ
بَنِينَ
وَبَنَٰتِۭ
بِغَيۡرِ
عِلۡمٖۚ
سُبۡحَٰنَهُۥ
وَتَعَٰلَىٰ
عَمَّا
يَصِفُونَ
١٠٠
Lakini walimfanyia Mwenyezi Mungu washirika, majini, ilhali Yeye ndiye aliyewaumba. Na wakamzulia kuwa ana wana wa kiume na wa kike, bila ya kuwa na elimu yoyote. Yeye Ametakasika, na ametukuka juu zaidi ya hayo wanayomuelezea kwayo!
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Ibn Kathir (Abridged)

Rebuking the Idolators

This Ayah refutes the idolators who worshipped others besides Allah and associated the Jinns with Him in worship. Glory be to Allah above this Shirk and Kufr. If someone asks, how did the idolators worship the Jinns, although they only were idol worshippers The answer is that i

…

Rebuking the Idolators

This Ayah refutes the idolators who worshipped others besides Allah and associated the Jinns with Him in worship. Glory be to Al

…
Tafsir Zaidi

Soma katika Muktadha

95. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mpasuaji nafaka na mbegu za tende, zikachipua. Humtoa aliye hai kutokana na maiti, na humtoa maiti kutokana na aliye hai. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu. Basi vipi mnadanganywa? 96. Ndiye anayepambaza mwangaza wa asubuhi; na ameufanya usiku kuwa mapumziko, na jua na mwezi kwenda kwa hesabu. Hayo ndiyo makadirio ya Mwenye nguvu kubwa, Mwenye kujua yote. 97. Na Yeye ndiye aliyewawekea nyota ili mwongoke kwazo katika giza mbalimbali za bara na bahari. Hakika tumezieleza kwa kina Ishara hizi kwa kaumu wanaojua. 98. Na Yeye ndiye aliyewaanzilisha kutokana na nafsi moja. Pako pahali pa kutulia na pa kupita njia. Hakika tumezichambua Ishara hizi kwa watu wanaofahamu. 99. Na Yeye ndiye aliyeteremsha maji kutoka mbinguni; na kwayo tukatoa mimea ya kila kitu. Na kutokana na baadhi yake tukatoa mimea ya kijani, tukatoa ndani yake punje zilizopandana; na kutokana na mitende katika makole yake yakatoka mashada yaliyo karibu; na mabustani ya mizabibu na mizaituni, na makomamanga, yanayofanana na yasiyofanana. Angalieni matunda yake yanapozaa na yakaiva. Hakika katika hayo kuna Ishara kwa kaumu wanaoamini. 100. Lakini walimfanyia Mwenyezi Mungu washirika, majini, ilhali Yeye ndiye aliyewaumba. Na wakamzulia kuwa ana wana wa kiume na wa kike, bila ya kuwa na elimu yoyote. Yeye Ametakasika, na ametukuka juu zaidi ya hayo wanayomuelezea kwayo!

- Swahili Translation - Rowad Translation Center

Endelea Kusoma

Maelezo na Tafakari

Huna maelezo au tafakari yoyote kuhusu aya hii.

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia