Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Al-Aaraf 7:72 فانجيناه والذين معه برحمة منا وقطعنا دابر الذين كذبوا باياتنا وما كانوا مومنين ٧٢

Ukurasa 159 · Juzuu 8

فَأَنجَيۡنَٰهُ
وَٱلَّذِينَ
مَعَهُۥ
بِرَحۡمَةٖ
مِّنَّا
وَقَطَعۡنَا
دَابِرَ
ٱلَّذِينَ
كَذَّبُواْ
بِـَٔايَٰتِنَاۖ
وَمَا
كَانُواْ
مُؤۡمِنِينَ
٧٢
Basi tukamwokoa yeye na waliokuwa pamoja naye kwa rehema zetu, na tukaikata mizizi ya wale waliozikanusha Ishara zetu, na hawakuwa wenye kuamini.
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Ibn Kathir (Abridged)

Allah mentions the rebellion, defiance and stubbornness of Hud'speople, and their opposition to him, peace be upon him,

قَالُواْ أَجِئْتَنَا لِنَعْبُدَ اللَّهَ وَحْدَهُ

(They said: "You have come to us that we should worship Allah Alone") Later on, the disbelievers of Quraysh said,

وَإِذْ قَالُواْ اللّ

…

Allah mentions the rebellion, defiance and stubbornness of Hud'speople, and their opposition to him, peace be upon him,

قَالُواْ أَجِئْتَنَا لِنَعْبُدَ

…
Tazama Tafsir

Soma katika Muktadha

65. Na kwa 'Aadi tulimpeleka ndugu yao, Huud. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu ila Yeye. Basi je, hamumchi? 66. Wakasema watukufu wa wale waliokufuru katika kaumu yake: Sisi tunakuona uko katika upumbavu, na hakika sisi tunakufikiria kuwa wewe ni katika waongo. 67. Akasema: Enyi watu wangu! Mimi sina upumbavu. Lakini mimi ni Mtume niliyetoka kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote. 68. Nawafikishia ujumbe wa Mola wangu Mlezi. Na mimi kwenu ni mwenye kuwanasihi, mwaminifu 69. Mnaona ajabu kukufikieni mawaidha yanayotoka kwa Mola wenu Mlezi kwa mtu aliye mmoja wenu nyinyi ili awaonye? Na kumbukeni alivyokufanyeni mshike mahali pa kaumu ya Nuhu, na akawazidishia katika umbo. Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu ili mpate kufanikiwa. 70. Wakasema: Je, umetujia ili tumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na tuyaache waliyokuwa wakiyaabudu baba zetu? Basi tuletee hayo unayotuahidi, ikiwa wewe ni miongoni mwa wakweli. 71. Akasema: Bila ya shaka adhabu na ghadhabu zimekwishakuwaangukia kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Mnabishana nami kwa sababu ya majina tu mliyoyaita nyinyi na baba zenu ambayo kwayo Mwenyezi Mungu hakuteremsha uthibitisho? Basi ngojeni, mimi pia ni pamoja nanyi katika wanaongoja. 72. Basi tukamwokoa yeye na waliokuwa pamoja naye kwa rehema zetu, na tukaikata mizizi ya wale waliozikanusha Ishara zetu, na hawakuwa wenye kuamini.

- Swahili Translation - Rowad Translation Center

Endelea Kusoma

Maelezo na Tafakari

Huna maelezo au tafakari yoyote kuhusu aya hii.

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia