Op die Dag zal iedere ziel worden beproefd met wat zij voorheen heeft gedaan en zij zullen worden teruggevoerd tot Allah, hun ware Heer, en wat zij plachten te verzinnen, zal van hen weggaan.
Tafseers
Lagen
Lessen
Reflecties
Antwoorden
Qiraat
Hadith
Katika kisimamo hiko cha kuhesabiwa, kila nafsi itazipekua na kuziona hali zake na matendo yake, na italipwa kulingana na hayo : yakiwa ni mema atalipwa mema na yakiwa ni maovu atalipwa maovu. Na wote watarejeshwa kwa Mwenyezi Mungu Aliye Muamuzi Muadilifu. Hapo watu wa Peponi watatiwa Peponi, na watu wa Motoni watatiwa Motoni, na vitawaondokea washirikina vile ambavyo walikua wakiviabudu badala ya Mwenyezi Mungu kwa kumzulia Yeye urongo.